Kura million 184 za online zawapa nafasi zaidi Justin Bieber na Tailor Swift tuzo za MTV EMAs 2012.


Justine Bieber na Tailor Swift  

Mwimbaji toka Canada Justin Bieber na mwanadada Tailor Swift ambae aliwahi kumake headlines zaidi baada ya kupokonywa tuzo mkononi na Kanye West kwenye MTV VMAs, juzi wawili hao wamefunika katika tuzo za MTV Europe Music Awards huko Frankfurt Ujerumani ambapo kila mmoja wao aliondoka na tuzo tatu idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya tuzo walizopata washiriki wengine huku zaidi ya kura million 184 zikipigwa online kuwachagua washindi mbalimbali.
Tailor Swift mwenye umri wa miaka 22 alishinda tuzo tatu ambazo ni Best Live, The Best Look na the Best Female. Swift alipata ushindani mkubwa sana hasa kwenye category ya the Best female ambapo alikuwa anashindana na Pink, Nick Minaj, Katy Perry na Rihanna .
Bieber yeye alionekana kupenya pia katika miondoko ya Pop ambapo alichukua tuzo ya Best Pop na Best World Stage trophies. Aliwashinda nominees wenzake kama Maroon 5, Ke$ha, Red Hot Chili Peppers na Tailor Swift. Mkali huyo anayewavutia vijana wengi wadogo kuingia kwenye muziki alinyanyua tuzo ya The Best Male award aliyokuwa anashindania na wasanii wakali na wenye uzito wajuu kwenye sanaa kama Jay-Z, Pitbull, Flo Rida na Kanye West.
Hivi karibuni Bieber aliachana na mpenzi wake Selena Gomez lakini yeye mwenyewe alipoulizwa kauli yake mara nyingi amekuwa akipata kigugumizi. Labda huu ushindi utampunguzia stress kidogo japo mapenzi yanasehemu yake tofauti na maisha ya muziki.
Hii ndiyo list kamili ya washindi wa MTV EMAs 2012:
•             BEST FEMALE: Taylor Swift
•             BEST SONG: Carly Rae Jepsen - "Call Me Maybe"
•             BEST MALE: Justin Bieber
•             BEST LIVE: Taylor Swift
•             BEST LOOK: Taylor Swift
•             GLOBAL ICON: Whitney Houston
•             BEST VIDEO: PSY - "Gangnam Style"
•             BEST WORLDWIDE ACT: Han Geng (Asia Pacific)
•             BIGGEST FANS: One Direction
•             BEST WORLD STAGE: Justin Bieber
•             BEST PUSH (for emerging stars): Carly Rae Jepsen
•             BEST ALTERNATIVE: Lana Del Rey
•             BEST ELECTRONIC: David Guetta
•             BEST HIP HOP: Nicki Minaj
•             BEST NEW: One Direction
•             BEST POP: Justin Bieber
•             BEST ROCK: Linkin Park

No comments:

Post a Comment