Sababu iliyofanya Steve RnB kufanya wimbo ambao sio RnB ' RnB'



Mkali wa R&B bongo aliyewahi kuingia kwenye top 5 ya wakali wa chorus TZ kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Leotainment, amefunguka kuhusu sababu zilizompelekea yeye kuachia wimbo aliomshirikisha Ommy Dimpoz ‘Radio’ ambao sio R&B na na hauna mahusiano ya karibu na R&B.
Katika interview aliyofanya na Leotainment, ‘The Tabasamu chorus Killer’ alisema sababu ambazo zilimpelekea yeye kuachia wimbo huo ni biashara tu na uamuzi wa kumshirikisha Ommy Dimpoz ni kwa sababu alitaka mashabiki Ommy Dimpoz wawe mashabiki wake pia.
“Unajua muziki sasa hivi yaani ni mpana sana, kwa hiyo kwa mimi nimeona kama ni nauwezo mkubwa sana wa kufanya nachoweza kufanya coz nilikuwa nahitaji pia mashabiki wa Ommy Dimpoz ambae ndiye niliyefanya nae kazi wawe pia mashabiki wa Steve R&B. So what I think kwamba mimi nilichofanya yani nimefanya biashara yaani bishara ya kimuziki ni vitu ambavyo vinaweza kufanyika pia kwenye game, kama ya industry ya muziki wetu unaweza kufanya kitu flani kwa ajili ya kuongeza mashabiki na kuonesha uwezo wako unaweza kufanya nini....” ni baadhi ya sentensi kibao alizofunguka Steve RnB.
Kuhusu issue ambayo wengi huwa wanazungumza kitaa kuwa the real R&B kwa bongo haiuzi kiivyo kama style nyingine na huenda ikwa ni sababu iliyopelekea Steve kuhamia hizi style za Nigeria na kudondosha ‘Radio’ na Ommy Dimpoz, alisema “sio kweli kiukweli nakataa coz mimi kilichonitambulisha ni R&B na sio muziki mwingine. Mi naweza kusema ni kubadilika tu.”
Steve aliwataja wasanii kwenye game Lady Jay dee na T.I.D ambao mwanzoni walikuwa wanafanya R&B lakini baadae wamebalika na kujichanganya pia na mitindo tofauti tofauti.
Kwa mujibu wa Steve R&B sasa hivi amehama management ya Zizzou entertainment na sasa yuko Combination entertainment ya Man walter ambayo ndiyo inafanya ngoma yake hii iliyotoka hivi karibuni, na pia ndiyo itakayosimamia project zake kwa sasa.
Steve R&B ni jina ambalo hutaacha kulitaja kama utaambiwa kutaja majina matano ya wasanii wanaofanya real R&B hapa Bongo na kusikika kupitia media kibao. Kwa kumbukumbu za haraka haraka Steve aliitwa R&B baada ya ku-kill ile chorus ya ‘Tabasamu’ aliyopewa shavu na Mr. Blue na baadae kuendelea kuua kwenye ngoma kibao za R&B ambazo zimempa heshima kubwa sana Bongo huku akiendelea kuzipendezesha chorus za wana Hip Hop pia.

No comments:

Post a Comment