Madaktari
wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye
lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa
vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili
kupata ukweli wa tukio hilo.
Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.
Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka ,
Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja
Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.
Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.
Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.
Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!
Imetolewa na
Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.
No comments:
Post a Comment