Maombi ya msanii wa filamu Elizabert
Michael (pichani kati ya askari) ya kuchunguzwa umri wake yameshindwa
kusikilizwa leo Mahakama Kuu Kanda ya dare s Salaam na kusogezwa mbele
hadi Julai 9, mwaka huu baada ya upande wa mashitaka kuomba maombi
yasisikilizwe leo.
Wakili wa serikali Elizabeth Kadanda
aliiomba Mahakama hiyo kuahirisha au kusitisha kusikiliza maombi hayo
leo kwasababu wamewasilisha maombi mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa
jaji anayesikiliza maombi hayo, Dk Fauz Twaib. Uamuzi uliopingwa ni
ule ambao Dk Twaib aliutoa Juni 11 mwaka huu kukubali kusikiliza maombi
ya kuchunguza umri wa Lulu ili kujua umri wake halisi baada ya kuwa na
utata upande wa mashitaka unadai Lulu ana miaka 18 wakati yeye anadai
ana miaka chini ya hiyo.
Baada ya maombi ya wakili Kaganda kuomba
maombi yasisikilizwe leo kwa sababu tayari amekatia rufaa uamuzi wa
jaji huyo, mawakili wa Lulu, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama
walisimama kwa nyakati tofauti na kuwasilisha hoja zao kuwa wanapinga
vikali maombi ya Kaganda. Walidai ni kinyume cha sheria kwa sababu
hakukuwa na amri yoyote kutoka mahakama ya rufaa kuzuia usikilizwaji huo
hata hivyo upande wa mashitaka ulionyesha kila dalili kuwa maombi leo
yatasikilizwa kwa kuwasilisha viapo pamoja na vielelezo vyao kama
mahakama ilivyowataka.
Walidai pia kuwa maombi hayo inaonyesha
yameifikia mahakama ya rufaa asubuhi hiyo ingawa walikiri huwa
yamesajiliwa na kupewa namba, walidai kuwa hiyo ni janja ya ofisi ya
mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuchelewesha. Baada ya kusikiliza hoja
hizo, Jaji Dk Twaib alitoa nafasi kwa wakili kaganda kujibu hoja za
upande wa utetezi hata hivyo Kaganda hakuwa na majibu ya hapo akaomba
nafasi kama yadakika kumi kujiandaa na kufanya mawasiliano na aliporudi
hakuwa na hoja zaidi ya kusisitiza maombi yake ya ahirisho kutoa nafasi
kwa mahakama ya rufaa kusikiliza maombi yao.
Jaji Dk Twaib katika uamuzi wake
alikubaliana na maombi ya Kaganda akisema kuwa kwakuwa maombi
yameshapokelewa na mahakama ya rufaa na kusajiliwa, wakati wowote
zitatakiwa mwenendo mzima wa kesi hivyo hana budi kuahirisha hadi Julai 9
mwaka huu. Uamuzi huo haukumfurahisha Lulu alilia huku akifuta
machozi baada ya kuona kuwa maombi hayo kwa siku hiyo yamegonga mwamba
hayatasikilizwa mpaka kusubiri amri ya mahakama ya Rufaa. Hata hivyo
jaji huyo alitoa amri nyingine kuwa haitakiwi mahakama ya Kisutu
kuendelea na kesi hiyo mpaka pale uamuzi utakapotoka mahakama hizo za
juu, uamuzi ambao ulipuuzwa kama alivyodai wakili Fungamtama kuwa Lulu
alipelekwa Kisutu na kesi ilitajwa katika jalada lililofunguliwa la
muda. Katika maombi hayo, tayari upande wa jamuhuri katika maandalizi
ya kusikiliza ulikuwa umeshawasilisha Mkanda wa video aina ya CD, yenye
mahohjiano kati ya mshtakiwa huyo na mtangazaji mmoja kuthibitisha
kwamba umri wa Lulu ni zaidi ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment