Siku
chache baada ya kuondolewa ndani ya kundi la Tip Tipo Connection, staa
wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Abdul Abubakar Chende ‘Dogo Janja’
ametua Bongo Muda mfupi uliopita akitokea A-town (Arusha).
Taarifa
ambazo zimeifikia blog hii kutoka pande za uwanja wa ndege wa JK
Nyerere zinasomeka kuwa Dogo Janja ametua mida ya saa 4:30 kwa pipa
(ndege) na kulakiwa na mashabiki wake wliojitokeza kwa wingi.
Akiwa
jijini Arusha kabla ya kuanza safarai yake hii ya leo jina Dogo janja
aliiposti kupita BBM maneno yaliyosomeka “Ki2 cha dua nini home lazima
kieleweke” akimaanisha kuwa yuko kwenye kuomba dua ili safari yake
ibarikiwe.
Dogo Janja ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi
na kusisitiza kwamba japo aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi kwamba zile zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu ambacho amekikubali kwa roho safi.
na kusisitiza kwamba japo aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi kwamba zile zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu ambacho amekikubali kwa roho safi.
Janja
amesema bado hajasaini mkataba mpya na WATANASHATI lakini kuna watu
wake wawili anaowasubiri kwa ajili ya kuja kuupitia pamoja huo mkataba,
baada ya hapo ndio atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza.
Amesema
amebadili mawazo na sasa atasoma Dar es salaam katika shule nzuri
ambayo aliahidiwa na Ostaz Juma meneja wa Watanashati, atakua anapelekwa
shule na kurudishwa nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni kusoma
kwenye shule binafsi nzuri na pia swala lake la muziki kuzingatiwa.
kwenye
sentensi nyingine amesema “sasa hivi nitakua naigiza na filamu pia na
kina Kitale manake tuko nao kwenye kundi moja la watanashati”
Kwa
kumalizia Janja amesema kauli mbiu ya wakati huu imebadilika “kauli
mbiu ya wakati nilivyokujaga nilisema nawakalisha matembo sasa hivi
nawalaza chali matembo”
No comments:
Post a Comment