Makundi matatu ya kigaidi Barani Afrika yameanza
kushirikiana katika harakati zao. Hii ni kwa mujibu wa Mkuu wa jeshi la
Marekani anayesimamia shughuli za usalama kanda ya Afrika. Jenerali
Cater Ham amesema kundi la Al Qaeda Afrika Kaskazini limekuwa
likiwasaidia wanachama wa Boko Haram nchini Nigeria na mabomu.
Akizungumza mjini Washington afisa huyo amesema
waasi wanaodhibiti kaskazini mwa Mali wameendelea kutumia eneo hilo
kuendesha harakati zao ikiwemo kupanga njama za kutekeleza
mashambulio.Jenerali Ham ni kamanda wa kitengo cha idara ya ulinzi ya
marekani kinachofuatilia masuala ya usalama barani Afrika{Africom} na
makao makuu yako Ujerumani.Tayari kuna wanajeshi 100 wa Marekani wanaosaidia kumsaka kiongozi wa waasi Uganda Joseph Kony ambao wanasimamiwa na kitengo cha Jenerali Ham.
Afisa huyo ametaja makundi hatari zaidi ikiwa ni pamoja na kundi la Al Qaeda Afrika Kaskazini{AQIM}, Boko Haram na Al-Shabab.
Ameongeza tisho kubwa ni kwamba makundi haya yameanza kushirikiana katika kufanikisha harakati zao.
Mapema mwaka huu nchi ya Mali ilishuhudia mapinduzi ya kijeshi na kufuatiwa na kudhibitiwa kwa eneo nzima la Kaskazini na makundi yanayotetea kujitenga ya Tuareg na wapiganaji wa kiisilamu.
No comments:
Post a Comment