Unaweza usiamini lakini huu ndiyo ukweli, Siku chache baada ya kutua
Bongo na kujiunga na kampuni ya Mtanashati Entertainments ya jijini,
nyota wa Bongo Fleva , Abdul Abubakar Chande ‘Dogo Janja’ mwishoni mwa
wiki iliyopita alisomea
kisomo maalumu cha kuomba Mwenyezi Mungu amnyooshee
mambo yake pindi atakapoanza kushusha ngoma mpya.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kisomo hicho kichoshudiwa na
Teentz.com, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ostaz Juma na Musoma alisema kuwa
wameamua kumfanyia kisomo hicho kwa lengo la kuweka kazi zote za Dogo
janja mikononi mwa Mungu kwa kuwa wana amini wao watu ambao
wajafurahishwa na mpango mzima wa dogo huyo kurejea Bongo
“Ni wazi kuwa wapo watu ambao hawajafurahishwa na kurejea kwa Dogo
Janja, na kama unavyojua binadamu wana hila zao ndiyo maana tumeamua
kufanya kisomo hiki ili kila kazi yake iwe kwenye mikono ya Mwenyezi
Mungu” alisema Ostaz Juma na kuongeza kuwa tulichokifanya ni kwa ajili
ya Mungu hivyo basi watu wasidili maneno na kusema tumefanya ‘ kafara’
alimaliza Ostaz.
Katika hatua nyingine baada ya kumalizika kwa kisomo hicho jana
(Jumapili) Dogo janja alifanya ‘shopingi’ ya nguvu kwenye maduka makubwa
ya viwalo yaliyopo Mlimani City jijini Dar.
Katika shopingi hiyo Dogo janja alitumia zaidi ya shilingi Milioni 2.5
za kibongo kununua vitu mbalimbali, kama Seti 5 za viatu, Suti 4, Jeans
10, T shirt 10,miwani 5, simu aina ya BlackBerry, Laptop na vitu vingine
kibao .
Huku akionekana mwenye furaha kubwa Dogo Janja aliiambia Teentz.com kuwa
amefuahi kwa kiasi kikubwa kwa yale yote ambayo Ostaz Juma na kundi
zima la Mtanashati kwa yote wanayomfanyia hivi sasa kwani hatakuwa na
malipo mengine zaidi ya kuwafanyia kazi nzuri zenye kiwango.
“Nina furaha sana, hakika namshukuru Ostaz kwa yote anayofanya kwangu
sina la kusema zaidi wasubiri ngoma za kweli zitakazokuwa kama shukurani
kwao kwa sababu ndiyo kitu pekee ambacho naweza kukifanya kwao” alisema
Dogo Janja.
No comments:
Post a Comment