NI SIKU MOJA IMEPITA YAN JUNE 26 TANGIA MARC VIVIAN FOE ALIONDOKA UWANJANI NA KUFARIKI DUNIA
Siku
ya 26 June 2003, mchezaji nguli wa Cameroon ambaye aliwahi kuchezea
mabingwa wa EPL 2011/2012, Manchester City, Marc Vivien Foe alidondoka
uwanjani na kufariki dunia dakika ya 72 ya mchezo wakati wa mechi ya
nusu fainali kombe la mabara dhidi ya Colombia katika uwanja wa Stade de
Gerland mjini Lyon, Ufaransa.
Awali kuna walioshauri Kombe la
Mabara na Uwanja wa Stade de Gerland viitwe jina lake, na huku kocha wa
zamani wa Man City, Kelvin Keegan akitangaza kwamba jezi namba 23
haitatumika tena klabuni hapo. Katika uwanja wa Man City, kuna jiwe la
kumbukumbu yake kama inavyoonekana ktk picha. Klabu yake ya kwanza, Lens
imeupa jina lake uwanja ambao uko karibu na uwanja wa FĂ©lix Bollaert
Stadium, ambapo na wao wakaamua kuifuta jezi namba 17 aliyoitumia
kipindi cha miaka mitano akiwa klabuni hapo.
Klabu yake
nyingine, Olympic Lyon nayo ikafuta kutumika jezi namba 17 aliyokuwa
akiitumia. Hata hivyo jezi hiyo ilikuwa inatumika mCameroon mwenzake
Jean II Makoun alipohamia Lyon kabla ya kifo cha Foe, hivyo yeye atakuwa
wa mwisho kuvaa jezi hiyo. Katika fainali ya kombe la mabara mwaka 2009
kati ya USA na Brazil, mtoto wake wa kiume wakiwa na miaka 14 wakati
huo alisoma ujumbe mfupi wa kumbukumbu ya baba yake.
MUNGU AMPUMZISHE KWA AMANI
No comments:
Post a Comment