Dereva wa magari ya Timu ya Ferrari Fernando Alonso
amekua dereva wa kwanza kushinda mara mbili mwaka huu kwa ushindi wa
kishindo kwenye mashindano ya Ulaya.

Fernando Alonso
Yeye Alonzo alianza katika nafasi ya 11 kabla ya
gari la usalama kuingilia mashindano kufuatia ajali lakini juhudi zake
zilimuezesha kupambana hadi nafasi ya nne.
Aliweza
kuongoza kufuatia mizengwe iliyotokea ndani ya kituo cha magari ya
McLaren ambako wakati wa kubadili tairi na kuongezea mafuta Hamilton
alipoteza zaidi ya sekundi 14 na kwa bahati nzuri dereva aliyekua
akiongoza Sebastien Vettel akashindwa kumaliza mbio hizo.
No comments:
Post a Comment