Shughuli za uokozi zinatarajiwa kuanza tena mashariki mwa Uganda ambako vijiji vitatu vilifunikwa na udongo
kufuatia maporomoka ya udongo yaliyokumba eneo la Bududa.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Uganda limesema kuwa zaidi ya watu kumi na wanane wamefariki dunia katika maporomoko hayo.Zaidi ya nyumba kumi na tano zimezikwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika eneo hilo.
Shirika hilo limesema maafisa wake wanaendelea kuwatibu waliojeruhiwa katika mkasa huo, katika eneo hilo lenye rutuba la Bududa, linalokuza kahawa na lililopo karibu na mbuga ya wanyama ya mlima Elgon.
No comments:
Post a Comment