Wahamiaji
haramu arobaini na wawili wamepatikana wakiwa wamekufa ndani ya lori
walimokuwa wakisafiria katika mkoa wa Dodoma, nchini Tanzania.
Naibu
waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Pereira Silima, amesema kuwa
watu hao waliokuwa wamesongamana ndani ya lori waliaga dunia kutokana
ukosefu wa hewa safi.
''Taarifa
tuliyopata ni kwamba kulikuwa na wasafiri waliokuwa wakisafirishwa
kwenye lori, ambalo lilikuwa kama kontena na halikuwa na hewa ya
kutosha''.Bwana Silima ameambia BBC.
wahamiaji walikuwa wanatoka Ethiopia
Amesema wahamiaji hao haramu kutoka Ethiopia walikuwa wakijaribu kuingia Malawi.
Kulingana
na bwana Silima wahamiaji hao walianza kufariki dunia wakiwa safarini.
Jihudi za wahamiaji hao kumjulisha dereva kuhusiana na hali yao
hazikufanikiwa, na hivyo kusababisha maafa ya watu arobaini na moja
ndani ya lori hilo.
Kulingana
na naibu waziri huyo wa mambo ya ndani tukio hilo lilifanyika Jumatatu
usiku. Na baada ya dereva huyo kugundua kuwa watu wamefariki, aliondoa
miili yao na kuitupa nje kabla ya kutoweka.
Mtu mmoja alifariki dunia akifanyiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Dodoma.
uhamiaji haramu umeenea
Polisi nchini wamesema wanamsaka dereva huyo ambaye alitoroka punde tu baada ya kushusha miili ya wahamiaji hao haramu.
Biashara
ya kuwasafirisha wahamiaji haramu hasa wanaotoka nchi za Somalia na
Ethiopia kupitia Tanzania imeenea sana. Wengi huelekea mataifa ya
kusini mwa Africa kutafuta maisha bora.
No comments:
Post a Comment