HII NDIO TIMU MPYA ILIYOMCHUKUA MICHAEL OWEN SASA HIVI.



.
Club ya soka ya Stoke City imethibitisha kwamba imempa mkataba wa mwaka mmoja mchezaji Michael Owen kuichezea club hiyo.
Michael Owen ambae amekubali hilo dili alilolipata akiwa ni mchezaji huru baada ya kumalizana na Manchester United, ameonyeshwa kufurahishwa kwa kupata tena nafasi ya kucheza kwenye English Premier League.
Michael mwenye umri wa miaka 32 aliichezea pia Man U kuanzia 2009 mpaka 2012 ambapo ni magoli matano tu ameyafunga kwa kipindi hicho.
.

No comments:

Post a Comment