Kiss aliyopigwa Rihanna yazidi kuzua utata, ‘did she feel it?’ Aliyemkiss aitolea maelezo, Drake & Chriss Brown waliishuhudia!!


Huyu jamaa na mkono wa kulia ulikuwa active!

Kati ya story zilizohit magazeti na mitandao mbali mbali wiki chache zilizopita ni habari zilizohusu matukio mengi sana yaliyojitokeza kwenye tuzo za video za MTV, yaani the MTV VMA ambapo mastaa wengi walipiga show kali kwenye stage moja.

Lakini tukio la rapper A$AP Rocky kumkiss the R&B queen Rihanna sio tu kuwa lilikuwa talk of the week lakini pia lilizua utata mkubwa na watu wamekuwa wakijiuliza kama lile tukio lilipangwa kama sehemu ya performance ya Rocky na Rihanna kwenye remix ya  "Cockiness (Love It)”, ama ni vipi.

Rapper Rocky amejitokeza na kuelezea nini kilitokea pale, ambapo yeye alipanda kuimba verse yake katika kumpa support mwanadada Rihanna ambae ndiye aliyefungua MTV VMAs kwa performance kali, Rocky aliwaushangaza umati wa watu pale alipomsogelea Rihanna wakati anamalizia verse yake na kumkumbatia kimahaba huku mkono wake ukiwa umemshika vizuri kabisa Rihanna kwa nyuma kwenye ‘steki’ kama wanacheza movie yenye title ‘hold me tightly’ halafu akampiga kiss shingoni, lakini Rocky anasema ilitokea tu na haikuwa ni idea iliyopangwa na wawili hao “it just happened” alisisitiza Rocky alipofanya interview na CBS Local.

Muda mchache kabla ya kupanda jukwaani kupiga show na Rihanna, Rocky alisema yeye hana uhusiano wowote na Rihanna zaidi ya uhusiano wa kibiashara. Na alipofaya interview na mtangazaji wa radio moja anaeitwa Bootleg Kev alisema ni kweli Rihanna is a cool chick, ila yeye ana girlfriend wake anaempenda.

Inasemekana kuwa alichokifanya Rocky huenda kiliwachanganya Chriss Brown na Drake ambao walikuwa seat za mbele kabisa hivyo kushuhudia kwa ukaribu zaidi, na watu waliokuwa karibu wamesema baada tu ya hilo tukio wote walionekana kushift in their seats uncomfortably. Drake na Chriss Brown hivi karibuni walifikia hatua ya kuzichapa na habari na ikasemekana pia kuwa chanzo ni huyu Rihanna.

Lakini swali lingine ni kwa Rihanna, ‘did she feel the Rocky’s kiss’ kwa sababu wakati Rocky anamsogelea kwa ukaribu Rihanna aliweka mikono yake miwili shingoni kwa maringo kama anataka kumhug Rocky, wakati Rocky anamkiss shingoni ndipo Rihanna alionesha kumpush Rocky kwa haraka na hata hivo Kiss ilikua ya haraka vilevile.

Angalia hiyo picha jinsi inavyotoa maelezo tata, wakati Rocky kama kanogewa na amefumba macho kwa hisia japo ni sekunde tatu hivi, Mkono wa kushoto wa Rihanna unamsukuma Rocky kimtindo, may be alishtukia kitu kama haikuwa planned kweli.

Baada ya hapo Rocky alishuka chini, na  Rihanna aliendelea na performance ya wimbo wake we found love, Tunasubiri majibu kutoka kwa Rihanna kuhusu kilichotokea, japo inaweza kuchukua muda kuyapata majibu haya but naamini one day the cover girl atafunguka kama story zitaendelea kuzagaa zaidi.

No comments:

Post a Comment