DMX amesema hajui kutumia computer kabisa, eti inamuogopesha hata kuiangalia!


DMX

Rapper mwenye sauti ya kipekee hasa kwenye miondoko ya Hip Hop DMX, ameweka wazi kuwa ameshindwa kabisa kuendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia kwa sababu hawezi kabisa kutumia computer, iwe desktop ama laptop.

DMX ambae ni member wa zamani wa kundi la Ruff Ryder amesisitiza kuwa  hana uwezo kabisa wa kutumia laptop wala desktop computer, kitu ambacho kwa ulimwengu huu sio cha kawaida hasa kwa mtu kama yeye mwenye jina kubwa na ambae habari zake nyingi zinazomhusu zinatokea sana kwenye mitandao mbali mbali.

Sio kwamba hana uwezo wa kujifunza zaidi kwa sababu elimu haina mwisho, lakini yeye hataki hata kujifunza kuhusu matumizi ya computer, na kila anapoiangalia computer anaona kama ina vitu vya kuogofya. Katika interview aliyofanya na Power 105.1 X alisema “angalia vitu vyote hivi, it’s scary, ina mambo mengi mno, naapa kwa jina la bibi yangu kweli tena hadi nashindwa kuwa mvumilivu kiasi hiki..Errr!ningeweza hata kuivunja” alisema DMX.

Hakuishia hapo akaongezea kuwa yeye kwake Google hata haina maana kabisaaa, na haimuingii akilini ni kama kichekesho flani, “it’s funny, it’s weird”.
Alipoulizwa yeye akitaka kuchek habari zinazomhusu yeye mwenyewe inakuaje kama anaogopa computer na hajui kuitumia, alisema yeye huwa anatumia simu yake na ndiyo anaielewa na sio laptop na desktop computer, “I know how to do it on a phone”.

DMX anaweza kuwa sio rappa pekee ambae ametamka hadharani kuwa hana ukaribu sana na hii teknolojia inayokuwa, wapo wengi ambao hata mambo ya tweeter kwao wanaona hayana maana, kama utakumbuka pia hasimu wa DMX kwa sasa na rapper wa Young Money Drake, aliwahi kukiri kuwa hakuwa na urafiki na internet enzi hizo bado anatafuta jinsi ya kutoka akiwa anafanya mixtape tu, hata nyimbo za 50 Cent na Kanye West alikuwa na CD zao na sio soft copies, lakini yeye alikiri jinsi internet ilivyomsaidia sana, ambapo nyimbo zilizokuwa kwenye Mixtape yake zilipoingia tu kwenye internet sauti yake ikakita kwenye sikio la boss wake wa Young Money Lil Wayne na kwa jinsi alivyomteka attention Lil Wayne akamsaka na kum-sign Young Money.
Haya kama hawa wa huko duniani ambao ndio huwa tunawaangalia na kufuata nyayo zao kwa kuamini wao wameendelea wanafeli hivi, je kuna usalama kweli kwa wasanii wa kibongo ambao baadhi yao hua wanaiga tu vitu bila kujali kama havina manufaa ilimradi kachukua kutoka kwa msanii wa marekani? Huu sasa ni wakati wa wasanii wetu wa Tanzania kuelimika na kuiga yale tu ya maana na yanayoweza kuwaletea maendeleo na kuachana na mambo mfano kama huu wa DMX.

No comments:

Post a Comment