Homa ya West Nile yaingia Serbia

Watu watatu wamekufa nchini Serbia kutokana na virusi vya homa ya West Nile ikiwa ni mara ya kwanza ugonjwa huo kutokea Serbia huku watu zaidi ya 30 wakiwa wanaugua.

Virusi vya West Nile huambukizwa na mbu ambapo huleta homa kama ya mafua, lakini inafikia kusababisha homa kali, kuzimia na ubongo kufura.
Wataalamu wanafikiri joto jingi la mwaka huu limesababisha kuzidi kwa mbu hao.
Mwaka huu, homa ya virusi vya West Nile ilitapakaa Marekani pia, kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tangu ugonjwa huo kuanza kutokea nchini humo mwaka wa 1999.

No comments:

Post a Comment