Goldie wa BBA Baada ya Kenya na Uganda, sasa Tanzania, apiga Collabo na AY


AY na Goldie

Weekend iliyopita siku ya Ijumaa aliyekuwa mshiriki kutoka Nigeria katika BBA Stargame Goldie aliwasili Tanzania akitokea nchini Uganda.
Itakumbukwa ziara yake ya East Africa ilianzia Kenya, na baadae alielekea Uganda ambako alifanya collabo na msanii wa hip hop Navio.

Goldie & Navio
Ujio wake wa hapa bongo umeonekana kuwa wa matunda kwa Ambwene Yesaya AY ambae amefanikiwa kufanya joint moja na mrembo huyo katika studio za MJ Records chini ya producer Marco Chali. Wimbo huo wa AY aliomshirikisha Goldie anategemea kuufanyia video mwezi November 2012 huko South Africa chini ya kampuni ile ile ya God Father waliohusika kutengeneza video yake iliyopita ya Party Zone.
Sam Misago na Goldie katika FNL ya EATV
Kama ilivyo kawaida kwa master wengi wanapotembelea bongo hupata nafasi ya kuvisit media houses tofauti for interviews, ndivyo ilivyokuwa kwa Goldie aliepata nafasi ya kuonekana live kupitia FNL Friday Night Live ya East Africa TV.

No comments:

Post a Comment