Ugonjwa wa moyo wamtesa Bebe Cool, asitisha ziara yake




Mwanamuziki wa Uganda Bebe Cool anasumbuliwa na maradhi ya moyo ambayo yamemlazimisha kusitisha ziara yake ya hivi karibuni.

Tatizo lake la moyo lilianza baada ya kupigwa risasi mwaka 2010 kwenye super market ya Nakumatt jijini Kampala, ambapo tangu hapo amekuwa na matatizo makubwa ikiwa pamoja na kusumbuliwa na ndoto za kutisha.

Hivi karibuni alipata mshtuko mbaya wa moyo nchini  Canada.

Kutokana na matatizo hatowez kufanya ziara yake ya nchni Marekani.

Kutokana na tukio hilo la kupigwa risasi Bebe Cool anaitaka serikali imlipe shilingi bilioni 2.9 za Uganda.

No comments:

Post a Comment