Mdudu wa All Stars ahamia Tanga chini ya Sumalee, EA Radio wazungumza wanavyouchukulia mtindo huu



Ule mwendelezo wa nyimbo za All Stars ndio kwanza umeenza. Baada ya Kigoma, tayari Mwanza, Morogoro na Mbeya wameshafanya. Bahati mbaya kwa mikoa mingine ukitoa Kigoma, nyimbo hizo zimeonekana kuwa za ‘kitoto’ na wengi kuziponda kwa kudai kuwa hazina hadhi ya Uall Stars bali ni copy and paste! 

Izzo B wa Mbeya amejikuta kwenye mzozo mkali  na wasanii wa mkoa huo  baada ya kutoukubali wimbo huo. Wasanii hao wamemshutumu Izzo B kuwa mbinafsi na kwamba anataka kushine yeye mwenyewe tu. Izzo anasema haiwezakani Mbeya All Stars bila wasanii kama Adili, Sugu na wengine.

Kwa upande wa Tanga,  Linex amemshawishi Sumalee afanye kitu cha Tanga na tayari ngoma hiyo imeshapikwa na Fundi Samweli wa Usanii Production. 

Tunaamini wimbo huo nao utaleta maneno mengi kama hizo za mikoa mingine zilivyopokelewa kwa shingo upande.


No comments:

Post a Comment