DITTO anawaomba mashabiki wake kumpigia kura katika Tunzo za radio ya Ufaransa RFI DISCOVERIES AWARDS 2012


Lameck Ditto
Lameck Ditto ni mmoja kati ya wasanii wanaozidi kuongeza wigo wa kazi zao za muziki katika soko la kimataifa. Amefanikiwa kuwa msanii pekee Africa mashariki alieingia katika Tuzo za Radio ya Ufaransa inayoitwa Radio France I international (RFI).

Ifuatayo ndio status aliyoiweka katika ukurasa wake wa facebook siku chache zilizopita:
“Nimefurahi kuwa mmoja kati ya Wanamuziki 10 Africa tuliochaguliwa Kushindania hii Tunzo ya RFI-France 24 Discoveries Award. Huko Nchini Ufaransa. Kunipigia Kura Ingia hapa~> : ... http://t.co/JCOTk3wo Piga Kura Ushindi Uje Tanzania......({})”
Hizi ni awards zenye lengo la kuutangaza muziki wa Africa, na msanii pekee wa Africa mashariki ambae amewahi kupata award hiyo ni Maurice Kirya wa Uganda mwaka 2012. Nchi zingine ambazo wasanii wao wamepata nafasi ya kuingia mwaka huu ni pamoja na Senegal, Nigeria, DRC, Namibia na zinginezo.
Ditto ameendelea kusisitiza wewe mtanzania uweze kumpigia kura na award ije Tanzania:

“Nipigie Kura katika RFI-France24 Descovery Awards hapa~ > http://mobile.english.rfi.fr/node/137503”.

Endapo Ditto atashinda licha kuwa atakuwa ameongeza kitu kikubwa katika CV yake ya muziki lakini pia atakuwa ameiletea heshima Tanzania. Hivyo kuna kila sababu ya kumpigia kura. 

Kwa msisitizo zaidi FUATA LINK HII HAPA CHINI KUWEZA KUMPIGIA KURA DITTO, kwani siku zilizotengwa kwa ajili ya kupiga kura ni kumi tu.

Link kwa ajili ya kupiga kura:

No comments:

Post a Comment