Sean Paul azungumzia rumors kuwa Jay-Z alimzuia kuperform na Beyonce ‘BABY BOY’ kwenye MTV VMA.


Sean Paul

Baada ya kutoka wimbo wa ‘Baby boy’ ambao sauti ya mkali wa miondoko ya dancehall ilisikika na ikimpa company the R&B queen Beyonce mwaka 2003, ilikuwa ni moja kati ya the best collaboration zilizohit radio waves kipindi hicho, na hivo kuwafanya watu waisubiri kwa hamu video ya wimbo huu ili wayaone makeke ya Beyonce na alivyocheza na Jamaican boy Sean Paul.

Surprisingly, katika video ya track hiyo iliyofanywa chini ya director Jake Nava, Sean Paul na pop queen Beyonce walionekana separately, na rumors zikazagaa mda mfupi tu kuwa Jay- Z alitoa masharti kwa Beyonce na Sean Paul wasishoot pamoja.

Sean Paul alipoulizwa kuhusu hii rumor katika interview aliyofanya na “Rap Fix Live” SP alisema:

 "The whole direction of the video was sold to me as, 'You're in a dream world,' " 

Beyonce
Hata hivo pamoja na kutokuwa na uamuzi kwa chochote alichokuwa anaelekezwa kwake haikuwa big deal, “It was not a big deal to me, but it really blew up into crazy stuff.” Alisema Sean Paul. Wakati Sean Paul hakupanda stage kumpa support Beyonce kuiimba “Baby Boy” katika tuzo za video za MTV za mwaka 2003, yaani 2003 MTV VMA, wimbo walioimba kwa kudakizana, zilitapakaa story kuwa Baba Blue Ivy, Jay-Z alimkataza Jamaica-born dancehall star kupanda jukwaa moja na Baby girl wake Beyonce Knowlance.

Lakini Sean Paul amekanusha hizo rumors katika interview hiyo, na alisema yeye amemfahamu Jay- Z hata kabla hajamfahamu Beyonce, “that’s a rumor that started , I’ have known Jay-Z from before I knew her” alisema SP.

Akikumbushia siku alipokuwa katika office za zamani za HOV’ Roc –A-Fella akipata lesson on on radio politics from the iconic MC. Sean Paul alisema watu tu ndo waliyakuza mambo, na yeye aliamua kuwa kimya kwa miaka yote hiyo kwa sababu anaamini it was doing its work. Na kwamba kulikuwa na mkanganyiko mwingi sana. 

Alimaliza kwa kuizungumzia ‘baby boy’ enzi za miaka hiyo 2003  na R&B queen Beyonce “she’s an amazing artist, the song was at number 1 for like nine weeks, so that was a very special time for me and for dancehall” alimaliza hivo mkali wa dancehall toka Jamaica

No comments:

Post a Comment