50 cent aitamani ‘body’ yake ya zamani; Baada ya music, movie, boxing sasa ageukia uandishi wa vitabu.




Kiongozi waa kundi la G- unit 50 Cent ambae alijikondesha ili kucheza movie ya All Things Fall Apart na kuleta uhalisia, hivi karibuni alitangaza mkakati wake wa kuurudisha mwili wake kuwa na muscles kama enzi zile ulivyoonekana kwenye cover ya album yake ya  Get Rich Or Die Trying mwaka 2003, iliyouza nakala kibao hadi kufikia mauzo ya mult-platinum.
50 Cent on Things fall apart
Mwili wake wa zamani anaotamani kuurudisha
50 cent alisema aliamua kujikondesha na alikuwa anakula vitu vya lojolojo tu tena mara tatu kwa siku hadi aliposhuka weight kwa kasi, tofauti na ratiba yake ya kula vizuri mara sita kwa siku burger na vyakula vingine vya kujenga mwili. Kama nilivyosema lengo la kujikondesha sana ilikuwa ni  kucheza clip moja kwenye movie yake ya All Things Fall apart ambayo inamuonesha akiwa kakonda sana baada ya kuugua, na kukutana na misukosuko mingi tofauti na alivyokuwa anaishi maisha ya raha na star wa kuaminika kwenye timu yake kwa nguvu na body lenye muscles.


Sasa ameamua kutengeneza upya mwili wake lakini hii itamtengenezea career mpya baada ya kuamua kuingia rasmi katika tasnia ya uandishi wa vitabu na anaanza kuandika kuhusu haya maisha yake ya fitness.
Katika Interview 50 ambae pia ni member wa The Money Team (TMT) alisema amekuwa akiandika vitabu kuhusu fitness tangu mwaka 2004, na akasema kwake concept ya strength iko kiakili, kimwili na kiroho pia, na anatarajia kuachia kitabu chake hivi karibuni, “probably the end of this year or the top of the next year.” Alimaliza 50 mjasiliamali anaewaza kuanzisha project mpya kila kukicha.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vya jijini New York, rapper huyo aliyezaliwa kwa jina la Curtis Jackson ameanza kufanya kikakati ili kitabu chake cha kwanza kiweze kuchapishwa January 2013 kitachoonyesha pia jinsi alivyojipunguza na jinsi ya kugain weight na bodya yake upya. Cover ya kitabu kinachotarajiwa kutoka cha 50 cent kimeonekana katika mitandao chenye tittle ‘Formula 50’.

Huyu ni mjasiliamali mwenye kila characteristics ya entrepreneur, Siku zote 50 cent amekuwa akiwaza kuwekeza katika kila kitu ambacho anaamini kitamuingizia mkwanja, baada ya kujiimarisha katika music, na kuingia katika tasnia ya filamu, 50 ameweza pia kugeuka promoter wa wacheza ndondi na kusaka vipaji vya watu wanaocheza ngumi hata kutoka Afrika, akishirikiana na rafiki yake wa karibu Mayweather.
Kila officiall album anayotoa 50 Cent hua inaambatana na movie yake baada ya muda, kama Get Rich Or Die Trying na Before I self Destruct, sasa kwa kuwa amejiingiza na kwenye uandishi wa vitabu labda anaweza kuja na wazo la kuandika vitabu vinavyohusu album zake kama anavyofanya kwenye movies, tusubiri tuone what is his next move.

No comments:

Post a Comment