Msanii Pipi Doreen sasa ni mama "Kingstone"


Pipi (mama Kingstone)
Pipi Doreen msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye nyota yake ya muziki ilianza ku'shine' kupitia wimbo wa "Njia Panda" alioshirikiana na Barnaba, ameingia kwenye orodha ya wasanii wa kike wa hapa Tanzania ambao wamebahatika kuwa na cheo kipya cha kuwa MAMA. 

Ijumaa ya September 14, 2012 Pipi alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume aliyempa jina la KINGSTONE. 

Haya ndio maneno aliyoyasema Pipi mwenyewe baada ya leotainment kumtafuta kwa lengo la kumpongeza kwa kujifungua.

"Sina mengi ya kusema bt sitaisahau tarehe 14 mwezi wa 9 mwaka 2012, kwani imenipa sababu ya kumpenda mama yangu mara mia zaidi na namshkuru Mungu kwa kuniwezesha kutimiza agizo la Mungu la kujifungua kwa uchungu".

Kwa mujibu wa reletionship status ya Pipi ya kwenye page yake ya facebook kusomeka "Engaged to Lucas Zuria", tunaamini soon tutakuja kuona imekuwa "Married". we wish you all the best Pipi katika majukumu mapya ya malezi ya mtoto wako.

No comments:

Post a Comment