Baada ya 50 Cent kutangaza kuirudisha G-Unit, Beyonce nae atangaza rasmi kundi lao la Destiny's Child


Mwaka huu umeanza vizuri kwa makundi ambayo fans wake walibaki na ndoto ya kurudi kwao yameibuka tena na kuzifanya ndoto hizo za fans wao kuwa kweli.
Siku chache baada ya 50 Cent kuwasapraiz fans na perfomance yake na member wa zamani wa G-Unit na baadae kutangaza kuirudisha upya, RnB Queen Beyonce Knowlence ametangaza rasmi kuwa destiny's child inarudi tena baada ya tetesi na matumaini ya kulirudisha kundi hilo kwa miaka nane hadi sasa.
Ikiwa ni wiki mbili tu kabla ya Beyonce kulishambulia jukwaa kwa show kali aliyojiandaa tangu mwaka jana ambapo atapiga show wakati wa halftime za Super Bowl February 3, amejitokeza hadharani na kutoa official announcement, "I am so proud to announce the first original Destny's child music in eight years!"
Queen Bey alisema ataliunda tena kundi hilo linaloundwa na swaiba wake Kelly Rowland na Michelle Williams (II) na wataachia album yao ya nyimbo zilizorekodiwa tangu mwaka 2004 ambayo itakuwa na wimbo mmoja mpya unaoitwa "Nuclear".

No comments:

Post a Comment