G-Unit yajiunga tena! 50 Cent Tony Yayo na wenzake wapiga bonge la show Puerto Rico.



Huu ni muungano wa kimya kimya, boss wa G-Unit 50 Cent ameungana na member wa zamani wa G-Unit Tony Yayo na wengine huko Puerto Rico na kupiga show kali kama surprise kwa fans wao.

Footage za muunganiko huo ambao haukutangazwa popote zilidondoka kwenye mtandao jumatano (January 9).

Curtis Jackson a.k.a 50 Cent na member wenzake wa G-Unit walirudi kimya kimya na kuwashangaza fans huku wakipiga bonge la shangwe walipomuona Tony Yayo na wenzake wakiwa na 50 Cent baada ya miaka mingi. G-Unit walilishambulia stage na ngoma zao kibao zilizohit kipindi kile na bado ni gumzo kwenye ulimwengu wa Hip Hop. Na hapo fans walipata zaidi ya kile walichokuwa wanategemea.

Kusambaratika kwa ngome ya zamani ya G-Unit kulilizorotesha kiasi flani kundi hilo na mara nyingi alisikika 50 Cent mwenyewe licha ya kuwa ameshawasign wasanii kadhaa kwenye lebel yake.

Mwezi november, DJ wa G-Unit (DJ Whoo Kid) alizungumzia jitihada zake za kuwashawishi member wa zamani wa G-Unit na 50 Cent kuirudisha ile G-Unit tena.

"I mean, hata sijui, nilijaribu kuongea nao. Fif alisema hajawahi kusikia lolote kutoka kwa Lloyd Banks, Sijui. Wanapaswa kutulia, sidhani kama wana matatizo makubwa. Kutokana na kile nachojua , wako poa. Walikuwa wote wakati wa mazishi ya Chris Lighty. Utasikia kutoka kwa 50 Cent mwenyewe. Atakupa picha nzima ya Banks na hali ilivyo na G-Unit. Lakini kutokana na kile nachojua , wako poa. Lakini 50 atakujulisha na kukupa maelezo zaidi kuhusu hali ilivyo." Alifunguka DJ Whoo Kid mwezi November.

No comments:

Post a Comment