Britney Spears aamua kuzitosa USD 15 Million kwa ku ‘quit’ u-judge wa X-Factor msimu ujao.



Inasemekana mwanamuziki  Britney Spears hatashiriki tena katika mashindano ya X-Factor msimu ujao ambayo amekuwa judge kwa msimu mmoja tu uliopita.
Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na Britney inasemekana pamoja na kuipenda sana show ya X-Factor lakini hivi sasa anataka ku-focus zaidi  katika muziki wake.

Lakini habari zaidi kutoka kwa watu wa ndani zinasema kuwa dalili za Britney kutoendelea na msimu ujao wa show hiyo zilianza kuonekana mapema mwaka jana wakati 'season one' ikiendelea kutokana na kukosolewa mara kwa mara kwa jinsi alivyokuwa aki judge washiriki.
Inavyoonekana Britney Spears anapata pesa nyingi zaidi katika muziki, kitu kilichompa nguvu ya kuamua kuzipa kisogo dola million 15 za kimarekani ambazo angezipata kwa kuendelea kuwa judge wa X-Factor.

Hivi sasa Britney Spears yupo studio akiendelea kurecord album yake ya 8 kwa msaada mkubwa kutoka kwa Will.i.am na producer Hit Boy.

No comments:

Post a Comment