Nas awaonya rappers wa kike wanaojipimanisha na wanaume kwenye sanaa, “Stop Playing Man’s Game When It Comes To The Artistic Sh*t”.




Rapper mkongwe Nas hivi karibuni amezungumzia msimamo wake kwa wasanii wa kike wanaofanya Hip Hop ambao wanajaribu kutafuta majina kwa kujiingiza kwenye utamaduni huo wakijiweka kama wanaume na kwamba itawagharimu sana kutoka na ku-shine wao kama wao.Japokuwa Nas anavutiwa sana na Emcees wa kike wanaong’aa kwenye game, amesema kuna msisitizo zaidi katika kujipimanisha na wasanii wa kiume.
 
Katika interview aliyofanya na hivi karibuni na jarida la Huck, Nas alisema, “nampenda Azealia Banks, nampenda Nicki Minaj. Hao wote ni wasichana ambao kwa sasa wapo kwenye game, ni muda wa wanawake katika hili game lakini wao wako katika illusion kwamba wanazuiwa, so women have to stop playing man’s game when it comes to the artistic sh*t. Wanatakiwa kwenda tu na kufanya game, waache kuogopa kuhusu wapi wanafit,” alifunguka Nas Escoba na kumalizia kwa msisitizo, “Just go and do it.”

No comments:

Post a Comment