Kris Kross wathibitisha kuungana tena, ni baada ya kimya cha miaka 21.


Kama ulikuwa unafuatilia muziki wa Rap miaka ya 90 sina shaka utawakumbuka vijana wawili Chris "Mac Daddy" Kelly na mwenzie Chris "Daddy Mac" Smith waliopata umaarufu miaka ile kama KRIS KROSS kwa kupitia hit song yao ya JUMP iliyoweza kukamata nafasi ya kwanza katika billboard hot 100 kwa wiki 8 mfululizo. 
Baada ya miaka 21 ya kutosikika wamethibitisha kulirudisha tena kundi lao na kuahidi kushiriki katika concert ya  maadhimisho ya miaka 20 ya recording lebel iliyowatoa ya So So Def inayomilikiwa na producer aliyegundua vipaji vyao Jermaine Dupri JD inayotegemewa kufanyika mwezi ujao February 2013.


Mac Daddy ndio huyo mwenye miwani aliyegeuza jeans yake nyuma kuwa mbele
Pamoja na mengi kubadilika kuwahusu wao ikiwa ni pamoja sasa hivi jamaa wameshakuwa watu wazima kama wanavyoonekana katika picha, lakini Mac Daddy bado anaitumia ile style yao ya kuvaa waliyokuwa wakiitumia miaka ile ya kugeuza nguo nyuma kama anavyoonekana katika picha hapo juu akiwa ameigeuza jeans yake nyuma mbele.

No comments:

Post a Comment