Justin Bieber aburuzwa mahakamani kwa kosa la kumpiga bodyguard wake na kumnyima malipo yake..!


Misala inazidi kumuandama 'baby hitmaker' Justin Bieber ambae hivi karibuni alikubwa na bad publicity baada ya picha yake akivuta bangi kusambaa kwenye mitandao, sasa ameburuzwa mahakamani na bodyguard wake wa zamani Moshe Benabou aliyemfanyia kazi kuanzia March 2011 hadi october 2012 akimtuhumu kwa kumpiga ngumi kadhaa kifuani wakati wamajibishano kati yake na mwimbaji huyo.

Katika mashtaka hayo pia, mlalamikaji amesema hakuwahi kulipwa na Bieber malipo yake ya over time japokuwa alikuwa kifanya kazi kwa muda wa saa 14 hadi 18 kwa siku.  Kwa hiyo anadai malipo ya fidia ya $ 421,261 kwa ajili ya malipo yake ya overtime, likizo na na wage benefit.
Mwanasheria wa bodyguard huyo alisema, "Kwa miaka takriban miwili Mr. Benabou alijitoa kikamilifu kuhakikisha usalama wa Mr. Bieber, hivyo Mr. Benabou alistahili kama waajiliwa wengine, kuwa treated kwa heshima, utu wake kwa mujibu wa sheria, unfortunately hakupata vyote hivyo."
Kwa upande wa Bieber hawakutoa tamko rasmi kujibu tuhuma hizo, lakini mtu mmoja wa karibu wa Justin Bieber aliliambia US Weekly kwamba mashtaka hayo hayana msingi wowote.

No comments:

Post a Comment