Justin Bieber ndiye mfalme wa Twitter, ni msanii mwenye followers wengi zaidi , amfunika Lady Gaga.



Justin Bieber msanii mwenye umri mdogo (18) anazidi kung'ara kwenye ulimwengu wa muziki na kuonesha kuwa na idadi kubwa sana ya mashabiki duniani huenda ikawa ni zaidi ya waimbaji wote waliohai. Sample hii inaonekana kwenye mtandao wa kijamii wa twitter kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi ya waimbaji wengine.

Hadi kufikia jumanne, January 22, Biebs alikua na wafuasi 33, 343, 647 katika akaunt yake, na kumfunika the Mother Monster ambae alikuwa anaongoza, lakini sasa ana wafuasi 33,315,459 na kushika nafasi ya pili. 

Kwa hali hiyo Justin Bieber ndie mfalme wa Twitter, lakini pia mwimbaji huyo toka Canada ndiye anaefatiliwa zaidi kwenye blogs mbalimbali pia hasa pande za Obama land akifatiwa na Lady Gaga.

Bieber na Gaga wote wanatarajia kuachia album zao mpya mwaka huu. Bieber atazindua album yake "Believe Acoustic" ilnatarajiwa kuingia sokoni January 29, wakati huo Gaga anatarajia kuachia album yake inayosubiriwa kwa muda mrefu na fans wake "ARTPOP".

No comments:

Post a Comment