Game ampiga shule Justine Bieber baada ya kupigwa picha akivuta bangi, asema kuna watu wa ngazi za juu wanavuta pia.



Rapper kutoka West Coast pande za Obama land The Game amezungumzia msala wa Justin Bieber  baada ya kupigwa picha akivuta bangi katika chumba cha hotel akiwa na rafiki zake baada ya kuachwa na mrembo wake Selena Gomez.

Game amemtetea Justine Bieber na kuomba asemehewe na media, na anaamini fans wake watamuonea huruma kidogo na kumsamehe kwa picha zake zilizooneshwa na media mbalimbali akivuta marijuana.

katika interview aliofanya na TMZ Game alisema, "Let's keep it real. Kuna watu wengi katika ngazi za juu ambao wanavuta weed kidogo. Sisemi kuwa ni poa, lakini Bieber alifanya kosa. Msameheni. Muacheni apitie njia yake ya maumivu katika ukuaji wake".
'One blood' hit maker akaamua ampige shule ya bure Justin Bieber ambae ni mdogo wake katika sanaa na kiumri pia (ana miaka 18).
"Na kama kweli Justin Bieber anataka kuvuta bangi, itamfaa zaidi akipata ruhusa ya daktari (prescription), kwa ajili ya matatizo ya macho kuwa na utandu(Glaucoma), ama tabia ya kusinzia hovyo (insomnia)." Huo ndo ushauri toka kwa rapper mgumu Game kwa Justine Bieber, lakini akakazia kwa mbadala wake kwa lugha ya ukakasi kidogo, "or else he can pull out of his ass on the fly."

No comments:

Post a Comment