Mchekeshaji Janeane Grofalo |
Katika hali ya kawaida watu hufunga ndoa wakiwa
wamekubaliana kwa asilimia 100 kuishi kama mke na mme kwenye shida na raha,
afya na ugonjwa. Lakini utimamu wa akili kwa asilimia 100 unahitajika katika
hili, na tilalila kupita kiwango flani hupunguza utimamu wa akili kwa asilimia
kadhaa.
Janeane Garofalo ambae ni mchekeshaji maarufu huko Marekani,
alienda New York kuhudhuria tamasha la wachekeshaji ‘The Ben Stiller Show”, na
huko alifunguka kuhusu ndoa yake na ex-husband wake ambae ni producer wa ‘Big
Bang Theory TV Show’ Robert Cohen kuwa walifunga ndoa miaka 20 iliyopita,
lakini hakuna hata mmoja kati yao alikuwa anafahamu kuwa ilikuwa ni ndoa halali
kwa sababu wote walikuwa tungi a.k.a tilalila wakati wa tukio hilo tena
kanisani.
Garofalo alisema yeye na mmewe walianza kudate tangu miaka
ya 90 na usiku mmoja wakiwa wamelewa walipitia kanisani huko Las Vegas na
kufunga pingu za maisha, na wote hawakuwahi kufikiria kuwa ile ndoa ilikuwa ni
halali hadi siku ambayo mwanasheria wa mmewe huyo wa zamani Cohen alipogundua
wakati Cohen wanajipanga kufunga ndoa nyingine ya halali na mtu mwingine baada
ya kuachana na mchekeshaji huyo ambapo kisheria iliwabidi watafute talaka ya
ile ndoa yao ya kilevi kwanza.
“Sisi tulidhani ulitakiwa kwenda mahakamani kusaini
makaratasi, so who knew?” Galofaro alinukuliwa na New York Post.
Galofalo na Cohen walitalakiana kisheria katika eneo la TD
Bank, Midtown dakika kadhaa kabla mchekeshaji huyo hajaingia kwenye tamasha
hilo, “Rob na Mimi tulikuwa na ndoa, kiukweli,na tumeimaliza kwa talaka dakika
30 kabla sijaingia hapa,” alifunguka Galofalo, na kumaliza kwa mshangao, “we
were married for 20 years until this evening!”
kwa kawaida talaka hua inafaida na hasara zake, ikiwa ni
pamoja na mtoa talaka kufidia baadhi ya gharama ama kugawa mali walizopata
wakiwa wawili, japo walikuwa hawajui kama ni wanandoa wawili hao sasa watapata
haki zao kwa kufaidika na mkwanja alioingiza kila mmoja wakiwa kama mke na mme
katika kushirikiana.
No comments:
Post a Comment