Lord Eyez, wakili wake na weusi wazungumzia kesi inayomkabiri, ahaahidi kuwasapraiz fans wake


Lord Eyez (kulia) akiwa na wakili wake wakati wakiongea na waandishi wa habari

Mweusi toka A- City, Lord Eyez amekutana na waandishi wa habari akiwa na wakili wake ili kuzungumzia kesi inayomkabiri ya wizi wa vifaa vya gari ambayo ili-make headlines sana siku kadhaa zilizopita.
Lord eyez amesema yeye kwa sasa anaiachia mahakama ambayo ndiyo itaweza kuchukua maamuzi ya kisheria kama yeye alihusika ama hakuhusika katika wizi huo wa vifaa vya gari.
Wakili wa msanii huyo anayejulikana kwa jina la Peter Kibatala amesema kesi hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye ndiye mhusika wa wizi wa vifaa hivyo lakini kwa sasa hivi wanaiachia kwanza mahakama ndiyo itakayoweza kuchukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi hiyo.
Hizi kauli za mweusi huyu na wakili wake zinaonekana zimepimwa na ruler ya kisheria kwa sababu ni kosa kisheria kujadili kesi ambayo iko mahakamani (commenting on a pending case).
Weusi nao walisema ‘neno’ kuhusu tuhuma zinazomkabili member huyo na kwamba tukio hili limewaathili hasa pale wanapokutana na watu mbalimbali na kusikia story toka kwa watu kwamba wote watakuwa wanahusika katika tukio hilo wakati ni story ambazo sio za kweli.
Kesi hiyo inatarajiwa kusomwa katika mahakama ya mwanzo jijini Dar es Salaam tarehe 13, 14 na 15 mwezi huu wa Novemba.
Hata hivyo the N2N soldier amesema kwa sasa anachotaka kufanya ni kudondonsha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya ‘surprise’ kwa mashabiki wake katika industry ya muziki wa Bongo.
Lord eyez alituhumiwa na msanii mwenzake Ommy Dimpoz kuwa alishirikiana na wenzake kumuibia vifaa vya gari lake na tuhuma hizo nzito ambazo ni pigo kwa kundi la weusi kiujumla zilipelekea Lord Eyez kukamatwa na kushikiliwa kwa na jeshi la polisi kwa siku kadhaa na baadae kufunguliwa kesi mahakamani ambapo alipewa dhamana.

No comments:

Post a Comment