Justine Bieber na Tailor Swift |
Mwimbaji toka Canada Justin Bieber na mwanadada Tailor Swift
ambae aliwahi kumake headlines zaidi baada ya kupokonywa tuzo mkononi na Kanye
West kwenye MTV VMAs, juzi wawili hao wamefunika katika tuzo za MTV Europe
Music Awards huko Frankfurt Ujerumani ambapo kila mmoja wao aliondoka na tuzo
tatu idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya tuzo walizopata washiriki wengine
huku zaidi ya kura million 184 zikipigwa online kuwachagua washindi mbalimbali.
Tailor Swift mwenye umri wa miaka 22 alishinda tuzo tatu
ambazo ni Best Live, The Best Look na the Best Female. Swift alipata ushindani
mkubwa sana hasa kwenye category ya the Best female ambapo alikuwa anashindana
na Pink, Nick Minaj, Katy Perry na Rihanna .
Bieber yeye alionekana kupenya pia katika miondoko ya Pop
ambapo alichukua tuzo ya Best Pop na Best World Stage trophies. Aliwashinda
nominees wenzake kama Maroon 5, Ke$ha, Red Hot Chili Peppers na Tailor Swift.
Mkali huyo anayewavutia vijana wengi wadogo kuingia kwenye muziki alinyanyua
tuzo ya The Best Male award aliyokuwa anashindania na wasanii wakali na wenye
uzito wajuu kwenye sanaa kama Jay-Z, Pitbull, Flo Rida na Kanye West.
Hivi karibuni Bieber aliachana na mpenzi wake Selena Gomez
lakini yeye mwenyewe alipoulizwa kauli yake mara nyingi amekuwa akipata
kigugumizi. Labda huu ushindi utampunguzia stress kidogo japo mapenzi
yanasehemu yake tofauti na maisha ya muziki.
Hii ndiyo list kamili ya washindi wa MTV EMAs 2012:
• BEST
FEMALE: Taylor Swift
• BEST
SONG: Carly Rae Jepsen - "Call Me Maybe"
• BEST
MALE: Justin Bieber
• BEST
LIVE: Taylor Swift
• BEST
LOOK: Taylor Swift
• GLOBAL
ICON: Whitney Houston
• BEST
VIDEO: PSY - "Gangnam Style"
• BEST
WORLDWIDE ACT: Han Geng (Asia Pacific)
• BIGGEST
FANS: One Direction
• BEST
WORLD STAGE: Justin Bieber
• BEST PUSH
(for emerging stars): Carly Rae Jepsen
• BEST
ALTERNATIVE: Lana Del Rey
• BEST
ELECTRONIC: David Guetta
• BEST HIP
HOP: Nicki Minaj
• BEST NEW:
One Direction
• BEST POP:
Justin Bieber
• BEST
ROCK: Linkin Park
No comments:
Post a Comment