Ripoti toka United States ndo zinatufungua macho watanzania
kuwa mwimbaji wa ‘what goes around comes around’ Justine Timberlake alikuja
Tanzania na mkewe Jessica Biel kimya kimya kwa ajili ya Honeymoon a.k.a
Fungate.
Wanandoa hao wapya walitua Kilimanjaro International airport
October 21, na wakaelekea Singita Grumeti ambayo ni private reserve ndani ya
hifadhi ya wanyama ya Serengeti ambayo iko mkoa wa Mara. Imesemekana kuwa wali-enjoy
vilivyo uzuri wa Tanzania katika hifadhi ya wanyama pori na walizunguka sana
kuona kila angle.
October 26 Justine Timberlake na mkewe walilala katika
Faru-Faru lodges na Singita Grumeti, kabla hawajarudi tena Kilimanjaro airport
October 30.
Inaonekana Jessica Biel ama Mrs. Timberlake anaizimia sana
Tanzania na ameona ndio sehemu nzuri sana ya kula raha na kupumzika, kwa sababu
hii siyo mara ya kwaza kwa mrembo huyo kuichagua Tanzania, January 2010 alikuja
Tanzania na akapanda mlima Kilimanjaro akiwa na wasanii wengine kama Emile
Hirch, Isabel I Lucas, Santigold, Lupe Fiasco, na wengine kibao na mission
ilikuwa ni kukusanya mkwanja na kuongeza ufahamu wa watu katika tatizo la
ukosefu wa maji safi linaloikumba dunia.
Justine Timberlake na Jessica Biel walifunga ndoa ijumaa
October 19, huko kusini mwa Italy. Walionekana kufurahia sana ndoa yao mpya na
kwa pamoja wakawaambia watu “it’s great to be married, the ceremony was
beautiful and it was special to be surrounded by family and friends.”
Mr& Mrs. Timberlake naamini ilkuwa poa pia kuitembelea
TZ na kucheki mazuri kibao tuliyopewa na Mungu na mtawambia na wengine kama
Timberland waje nao sio kwa show tu hata kutembea na kula good time.
Kutokana na ujio wao wa
kimya kimya haikuwa rahisi kwa waandishi wa habari kupata picha zao
wakiwa Tanzania sababu hakuna aliyefahamu.
No comments:
Post a Comment