Mkasa wa mapenzi yenye pembe tatu zinazowahusisha warembo
wawili Rihanna na Karrueche Tran kwa 'Don’t wake me up' hit maker Chris Brown
unazidi kunoga siku hadi siku na imesemekana kuwa warembo hao wako poa tu na
maisha yao na ‘baby boy’ wao Chris Breezy.
Mtu mmoja ameiambia Hollywood Life, “he got them both
twisted up. He is trying to get as much p-y as he can before he leaves next
month.”
Chanzo hicho kiliendelea kufunguka, “Chris anawapenda kweli
wote na wanajua hilo na wao wanampenda pia”, akaendelea, “it’s crazy situation.
Na inafanya kazi kwao, na ni kama RiRi na K.T wako poa tu na hili, hivo ndivyo
ilivyo.”
Lakini stori za mtaa kwa upande mwingine zilisema Rihanna
aliogopa pale alihisi kuwa labda Chris angeenda na Karrueche T kwenye party
yake kubwa ya Halloween iliyowakutanisha mastaa kibao jumatano ya wiki hii.
Mtu mmoja alisema, “ingawa the 'umbrella' hit maker RiRi
alikuwa poa tu kwa kile kinachoendelea kati ya Chris B na K.T lakini hakuwa na
uhakika kama Chris ataamua kwenda kwenye party yake na K.T na hii ni kutokanana
tetesi ambazo zilikuwa zimetapakaa mitaani na kwenye mitandao kuwa huenda Chris
akatokea pale akiwa na K.T kama kawaida. Hapo ndo utaona kweli mapenzi ya
watatu hayawezekani hasa inapoonekana kuwa itabidi kukutana kwenye eneo moja.
Chis Brezzy alitangaza kuachana na Karrueche October 4, na
kauli yake ilikuwa ,” nimeamua kuwa single ili nifocus kwenye kazi yangu.
Nampenda sana Karrueche lakini sitaki kumuona anaoumia kwa sababu ya urafiki
wangu na Rihanna. Badala yake inabidi niwe single ili Kurusu kila mmoja wetu
kuwa na furaha.”
Siku chache zilizofuata Chris B alitoa video ikiwa na kauli
nyingine inayoonesha kweli anawapenda wote Rihanna na Karueche na hajui afanye
nini na hajui kama kweli inawezekana kuwapenda watu wawili lakini ndivyo yeye
anavyojisikia, lakini mwisho wa siku ikaonekana kabisa ameamua kuhamia rasmi
kwa Rihanna wake wa zamani na kumtangaza rasmi japo ndo hivyo tena hawaachani
na Karrueche pia.
Haya ndiyo yanayoitwa Triangular Love, “mapenzi ya pembe
tatu”.
No comments:
Post a Comment