Yakiwa yamebaki masaa machache wananchi wa Marekani waanze
kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo kwa awamu nyingine, visa na mikasa ama
vituko vimezidi kutawala katika kampeni za uchaguzi huo labda ni mzuka wa
kuonesha hisia za watu tofauti tofauti kwa yule wanaemsapoti na kumponda
wasiyemsapoti.
Hivi karibuni watu wanaosadikika kuwa ni wapinzani wa rais
Obama wametoa toilet paper zenye sura yake na T.P hizo zikasambaa maeneo ya
firestation huko Florida.
Ripoti zinasema toilet paper hizo zimetolewa kujibu
mashambulizi baada ya mfanyakazi mmoja wa kituo hicho cha zimamoto aliziondoa
sticker zote zinazompinga Obama ambazo zilikuwa zimewekwa kwenye maeneo ya umma
na sio maeneo ya watu binafsi ama mali binafsi.
Hata hivyo toilet paper hizo nazo zimeondelewa maeneo hayo
na kupigwa marufuku maeneo hayo ya Florida firestation kwa sababu ni maeneo ya
umma (public place) na sio maeneo binafsi.
Hivi karibuni zilisambaa T-shirt zenye maneno ya kumpinga
mpinzani wa Barack Obama katika kinyang’anyiro hicho cha urais wa taifa kubwa
duniani Mitt Romney, t-shirt hizo zilizotengenezwa na vizuri kwa ushirikiano wa
madesigner watatu John Searles, Aaron Rhodan na Julian Streete zina maandishi
yanayosomeka, “That Mitt I Don’t Like.”
Siku ya jumanne November 6, ikiwa na maana kwamba ni masaa
machache tu kuanzia sasa raia wa Marekani watapiga kura kumchagua rais wa
tiaifa hilo na hapo ndipo maoni ya wengi yatashinda. Ni Romney ama ni Obama
tena? Kura ndiyo muamuzi wa mwisho, hizi nyingine za kutoleana T-shirt na
kuwekana kwenye toilet paper ni mbwembwe tu na mizuka ya baadhi ya watu ili
kushawishi watu wengine kujiunga nao na kufata maoni yao.
No comments:
Post a Comment