Anaitwa Major Harris…aliyekuwa member wa kundi la muziki wa
soul kutoka Philadelphia “The Delfonics” ameripotiwa kufariki dunia huko
Richmond, Virginia.
Vyombo vya habari vya karibu vimeripoti kifo hicho kutokea
ijumaa Nov 09 kutokana matatizo ya moyo aliyokuwa nayo muda mrefu na kushindwa
kufanya kazi kwa mapafu ambako kulipelekea kukimbizwa hospitali na baadae
kufariki dunia.
Kihistoria Major Harris alianza muziki long time..mwishoni
mwa miaka ya 50’s na aliwahi kuwa member wa makundi kibao tu kama Charmers,
Frankie Lymon’s Teenagers na Nat Turner’s Rebeillion kabla hajamalizia muziki
wake The Delfonics mwanzoni mwa 1970’s ambapo walitengeneza hits kama “La-La
(Means I Love You) and “Didn’t I (Blow Your Mind This Time)”.
Wasanii kibao wa HipHop wa mid era wame-sample ngoma kibao
za The Deflonics…baadhi yao ni pamoja na Grand Puba “Very Special”, Ghostface
Killah “Holla” & “R.A.G.U.” na Fugees “Ready or Not”..R.I.P Major Harris.
No comments:
Post a Comment