Ule msemo wa nabii hakubaliki kwao umethibika kwa mwimbaji
anaefunika katika majukwaa ya kimataifa Justin Bieber ambae alijikuta akizomewa
wakati anajiandaa kupanda jukwaani kuimba wakati wa mapumziko katika mchezo wa
mpira wa miguu huko nchini kwao.
Crowd ya Toronto ilianza kuzomea kwa nguvu baada tu ya
kumuona Bieber kwenye screen kubwa ya uwanjani akiwa anasogea jukwaani kuimba
hit songs zake mbili ‘Boyfrriend’ na ‘Beauty and Beat’.
Mashabiki hao walizomea tena pale ambapo jina la Bieber
lilitajwa na MC uwanjani hapo. Bieber ambae ni mshindi wa American Awards kama
msanii wa mwaka alionekana kutoteteleka na kuzomewa na akaendelea kupiga show
hadi mwisho tena kwa nguvu ile ile.
Japokuwa watu walizomea tangu mwanzo hadi mwisho wa
performance yake muda wote wakati timu ziko katika mapumziko, alimaliza nyimbo
zote mbili bila kuonesha hisia yeyote mbaya kwa mashabiki, na Mcanada huyo
alimalizia na sentensi mbili, “Thank you so much Canada. I love you.”
Mmoja kati ya football fans waliokuwa pale walielezea kwa
nini watu walimzomea Biebs, “J-Biebs hashangilii mpira wa miguu, unajua, wala
Carly Rae Jepsen pia,” alisema Ryan Prisque (22), shabiki toka pande za
Calgary.
Ingawa Justin Bieber ni msanii mwenye umri mdogo anastahili
kusifiwa kwa kuweza kuhimili changamoto kubwa kama hiyo na kuonesha
anavyoiheshimu kazi yake na hisia za mashabiki wake iwe ni hisia positive ama
negative, hilo ni moja kati ya vigezo vya ukomavu katika sanaa.
No comments:
Post a Comment