Mhadhiri (lecturer) wa chuo kikuu cha Mtakatifu
Augustino ama SAUT, Mwanza, ameguswa na
mashairi ya ngoma ya Fareed Kubanda a.k.a Fid Q yaliyopo kwenye ngoma yake
MWANZA MWANZA.
Denis Mpagaze, mtaalam wa masomo ya journalism and
communication research, mwandishi wa vitabu na journals mbalimbali na mjuzi wa
mambo ya falsafa, amewashangaza wanafunzi wake ambao wamezoea kukuta matangazo
mbalimbali kwenye page yake ya facebook yanayohusu masomo na quotation za
waandishi maarufu wa vitabu.
Tofauti na siku zote, wanafunzi wake wamekutana na
maandishi yanayosema, “‘‘USIJARIBU KUPIMA KWA SHINGO UKALI WA UPANGA AU KUIMBA
UNAKULA KARANGA NA SUMU KWA KUILAMBA...MANENO NI MKUKI, HEKIMA NGAO... (FID Q)
Kitendo cha mhadhiri huyo kukubali uandishi wa Fid Q,
unadhihirisha jinsi mashairi yake yalivyotukuka, hata ukizima beat na snare
bado maneno anayotumia yanaweza kupenya na kugusa vichwa kama hivi katika vyuo
vikuu.
Mwenyewe Fid Q aliwahi kusema, ‘nasikika hata
ukini-mute.’
Kutokana na status ya mhadhiri huyo, maswali kibao
yalizuka, “Kumbe unapenda mistari ya wana hip hop sir? Aliuliza dada mmoja
anaeitwa Neema Nyange.
Na mwingine aitwaye Deogratias Konyani alisema, ‘Dah!
Falsafa za kitaaolojia by Fid Q! Hip hop unaipenda sir?’ huku Maulid Mombo naye
akiungana na wenzie kuuliza,’Dah ticha umenifurahisha kumbe na we umo safi bt
umesikia kitu kipya cha fid q-Sihitaji rafiki ?’ na Garma Paul kuchangia,
‘ticha we mwana hip hop nini?’
Kutoka na maswali hayo, mhadhiri huyo akajibu kwa
kusema, ‘Namaanisha kimaisha, kwenye fani ukiwa na akili unatoka vizuri sana na
haraka, kwenye vitabu hata uwe committed kiasi gani unakuja kutoka uzeeni’
Does this mean huyu mwalimu anatamani kuingia kwenye
game ili afikishe alichoandika kwenye vitabu kwa wahusika haraka zaidi? I can’t
tell, ila alikili kuwa anayo album ya Fid Q tayari mkononi na ili kudhihirisha
kuwa anayajua mashairi kibao ya NGOSHA aliandika, ‘Akupigaye ngumi ya jicho na
we mpige ya sikio, akikuuliza unaonaje na we muulize unajiskiaje.....ni vigumu
majivu kuwa mkaa..’
No comments:
Post a Comment