Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa benki ya Barclays,
moja ya benki kubwa zaidi nchini Uingereza, atahojiwa na kamati maalum
ya bunge hii leo.
Bwana Bob Diamond, ambaye alijiuzulu hiyo jana anatarajiwa kuhiojiwa kuhisana na sakata ya kuongezwa kwa viwango vya riba iliyopelekea kujiuzulu kwake.
Diamond, alijiuzulu hiyo jana baada ya benki ya Barclays kushutumiwa vikali kwa kuhujumu na kuongeza viwango vya riba kinyume cha sheria.
Benki hiyo imepigwa faini mabilioni ya dola kufuatia kashfa hiyo.
Waandishi wa habari wanasema, Bwana Diamond atahojiwa kuhusiana na mazungumzo aliyofanya na naibu gavana wa benki kuu, wakati viwango hivyo vya riba viliongezwa.
No comments:
Post a Comment