Barabara za juu kwenye miji ya wenyewe.
Waziri wa ujenzi John Magufuli wakati akisoma bajeti ya wizara yake bungeni July 5 2012 amesema kiasi cha shilingi milioni 577 kimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Ubungo Maziwa, External, Tabata, Dampo na Kigogo.
Milioni 1000 ni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami Kimara, Kilungule na External, ambapo milioni elfu 2 zimetengwa kwa ajili ya barabara ya Mbezi, Maramba Mawili pamoja na barabara iendayo shule ya msingi Maramba mawili, Kinyerezi na Banana.
Milioni nyingine elfu mbili mia moja ni kwa ajili ya barabara ya Tegeta Kibaoni, Wazo Hill, Goba, Mbezi na Morogoro, Milioni elfu moja imetengwa kwa ajili ya barabara ya tangi bovu goba na Goba ambapo milioni 573 ni kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya kimara Baruti, Msewe, Changanyikeni ambapo pia Magufuli amesema Wizara yake pia kupitia TANROADS imetenga bilioni 18 kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam.
Kwenye line nyingine, Magufuli amesema barabara za mikoa zimetengewa shilingi milioni 20 na 410 zote zikiwa fedha za ndani ambapo kilichopangwa kutekelezwa ni kufanya ukarabati wa jumla ya ukarabati wa jumla ya kilomita 337 kwa kiwango cha changarawe na kujenga kilomita 23.7 kwa kiwango cha lami.
Ujenzi wa maegesho ya vivuko katika mwaka wa fedha 2012/2013 Magufuli amesema zimetengwa shilingi milioni elfu nne na mia nane ambapo wizara yake inaendelea na juhudi za kuanzisha usafiri wa boti, kivuko katika mwambao wa bahari ya hindi kuanzia Dar es salaam hadi Bagamoyo ambapo zimetengwa pia shilingi milioni elfu mbili.
No comments:
Post a Comment