Serena Williams kutoka Marekani amemshinda Agnieszka
Radwanska wa Poland 6-1 5-7 6-2 kujishindia taji la wanawake la
mashindano ya kila mwaka ya Wimbledon.
Hii ni mara ya tano kwa Serena kushinda
mashindano haya, ikiwa ni mara yake ya 14 kushinda mashindano ya kiwango
kikubwa kama hiki(Grand slam).Serena alianza vizuri kwa kitisho seti ya kwanza akionyesha dalila za kumaliza kazi kwa haraka alipomchapa Radwanska 6-1 seti ya kwanza iliyomalizika kwa mda mfupi kuliko ilivyotarajiwa.
Hata hivyo mambo yalibadilika katika seti ya pili wachezaji hawa waliporejea baada ya kukwepa mvua iliyosababisha mechi kusimama kwa mda wa dakika 25 .
Seti ya tatu ilipoanza, Serena lionyesha ukomavu wake na uzowefu kwa kumdhibiti mpinzani na kutumia kila mbinu alizo nazo akiweka rekodi ya ''ace'' kupiga mashuti ya mpira bila kuguswa, na sasa ametimiza 'ace' 100 akimpita Philipp Kohlschreiber wa Ujerumani ambaye anashikilia rekodi ya ace 98.
Kabla ya pambano la leo Serena alikua na jumla ya 'ace' 85, kwa hiyo katika mechi ya leo ametumia ace'15 kuweza kumpiku raia wa Poland.
Hivyo ndivyo Serena alivyoweza kuuchangamsha uwanja wa Wimbledon na kunyanyua ngao ya 'rosewater dish' inayowaniwa na wanawake kwenye uwanja wa Wimbledon kila mwaka.
No comments:
Post a Comment