NEWZ:MGOMO WA WALIMU KUTIKISA TENA TANZANIA NDANI YA SIKU TATU ZIJAZO



Wakati bado ishu ya mgomo wa Madaktari bado iko akilini mwa Watanzania, Chama cha walimu Kigoma kimeonya mwalimu yeyote atakaejaribu kufanya usaliti wa mgomo wao usio na kikomo kwa walimu wote Tanzania unaotarajiwa kuanza siku tatu zijazo.

Katibu wa CWT Kigoma Emmanuel Samara ametoa hiyo tahadhari wakati alipokutana na wawakilishi wa walimu kutoka shule 240 za wilaya ya Kasulu na kuamplfy kwamba katika mgomo wa mwaka 2008 baadhi ya walimu waliwasaliti wenzao na kutoshiriki Mgomo jambo ambalo hawatoliruhusu litokee tena mwaka huu.

Amesema “Mgomo umeitishwa na chama cha wafanyakazi kwa mujibu wa katiba ya chama na walio wengi wameunga mkono, wanachama wetu mashuleni watapiga kura ya kutaka mgomo au kutokutana, hatutaki huu mgomo uwe ni wa chama cha walimu .. uwe ni mgomo wa wafanyakazi wenyewe kwa kuamua kwa kura” – Samara
“Nawatahadharisha kwamba hivi ni vita, katika vita msaliti anaweza asionekane kabisa maisha yake yote kwa sababu na sisi wengine Makamanda wa vita yanayotupata ni makubwa nadhani mnajua kilichompata Ulimboka Kule Dar es salaam… sasa siwezi kukubali nife au niumizwe kwa sababu tu flani kanisaliti, haiwezekani” – Samara

Kwenye line nyingine Mwenyekiti wa CWT mkoani Kigoma Said Ndee amesema mgomo wao ni wa kisheria na umeandaliwa kisayansi ili kuwafanya kufanikisha malengo yao na kwamba kama serikali haitokubali kufikia muafaka kwenye mazungumzo yanayoendelea hakuna atakaewarudisha nyuma kwenye hii ishu.

No comments:

Post a Comment