Mkali wa R&B bongo aliyewahi kuingia kwenye top 5 ya
wakali wa chorus TZ kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Leotainment,
amefunguka kuhusu sababu zilizompelekea yeye kuachia wimbo aliomshirikisha Ommy
Dimpoz ‘Radio’ ambao sio R&B na na hauna mahusiano ya karibu na R&B.
Katika interview aliyofanya na Leotainment, ‘The Tabasamu
chorus Killer’ alisema sababu ambazo zilimpelekea yeye kuachia wimbo huo ni
biashara tu na uamuzi wa kumshirikisha Ommy Dimpoz ni kwa sababu alitaka
mashabiki Ommy Dimpoz wawe mashabiki wake pia.
“Unajua muziki sasa hivi yaani ni mpana sana, kwa hiyo kwa
mimi nimeona kama ni nauwezo mkubwa sana wa kufanya nachoweza kufanya coz
nilikuwa nahitaji pia mashabiki wa Ommy Dimpoz ambae ndiye niliyefanya nae kazi
wawe pia mashabiki wa Steve R&B. So what I think kwamba mimi nilichofanya
yani nimefanya biashara yaani bishara ya kimuziki ni vitu ambavyo vinaweza
kufanyika pia kwenye game, kama ya industry ya muziki wetu unaweza kufanya kitu
flani kwa ajili ya kuongeza mashabiki na kuonesha uwezo wako unaweza kufanya
nini....” ni baadhi ya sentensi kibao alizofunguka Steve RnB.
Kuhusu issue ambayo wengi huwa wanazungumza kitaa kuwa the
real R&B kwa bongo haiuzi kiivyo kama style nyingine na huenda ikwa ni
sababu iliyopelekea Steve kuhamia hizi style za Nigeria na kudondosha ‘Radio’
na Ommy Dimpoz, alisema “sio kweli kiukweli nakataa coz mimi
kilichonitambulisha ni R&B na sio muziki mwingine. Mi naweza kusema ni
kubadilika tu.”
Steve aliwataja wasanii kwenye game Lady Jay dee na T.I.D
ambao mwanzoni walikuwa wanafanya R&B lakini baadae wamebalika na
kujichanganya pia na mitindo tofauti tofauti.
Kwa mujibu wa Steve R&B sasa hivi amehama management ya
Zizzou entertainment na sasa yuko Combination entertainment ya Man walter
ambayo ndiyo inafanya ngoma yake hii iliyotoka hivi karibuni, na pia ndiyo
itakayosimamia project zake kwa sasa.
Steve R&B ni jina ambalo hutaacha kulitaja kama
utaambiwa kutaja majina matano ya wasanii wanaofanya real R&B hapa Bongo na
kusikika kupitia media kibao. Kwa kumbukumbu za haraka haraka Steve aliitwa
R&B baada ya ku-kill ile chorus ya ‘Tabasamu’ aliyopewa shavu na Mr. Blue
na baadae kuendelea kuua kwenye ngoma kibao za R&B ambazo zimempa heshima
kubwa sana Bongo huku akiendelea kuzipendezesha chorus za wana Hip Hop pia.
No comments:
Post a Comment