Rich Oganiru |
Kwa watazamaji wa filamu za kinaijeria, sura ya Rich
Oganiru si ngeni machoni.
Ni muigizaji maarufu wa filamu hizo na tayari
ameshaigiza zaidi ya filamu 300.
Kwa mujibu wa jarida la National Enquirer la Nigeria, Oganiru
anakabiliwa na kesi nzito ya mauaji ya mke wake mfanyabiashara bilionea aliyekuwa
akiishi Abuja.
Huyo hakuwa mke wake wa kwanza kwani mke wake wa awali
naye alikufa katika mazingira yasiyoeleweka miaka kadhaa iliyopita.
National Enquirer limedai kuwa muigizaji huyo alikuwa akiishi
maisha duni kabla ya kukutana na mwanamke huyo mfanyabishara aliyebadilisha
maisha yake.
Inadaiwa kuwa baada ya kifo cha mke wake aliyezaa naye
watoto wawili wa kiume, alijikuta katika maisha magumu kiasi cha kukosa hata
hela kununua chakula na ndipo alipokutana na mwanamke huyo aliyemwimbisha na
kueleweka hasa kutokana na sura yake kuwa maarufu kwenye filamu.
Ripoti inasema kuwa baada ya kuishi pamoja na kuoana na
mwanamke huyo, Rich alianza kulalamika baada ya mkewe kushindwa kushika mimba.
Inaendelea kudai kuwa mke wake alimwamini na kumfanya
awe mmiliki wa baadhi ya mali zake na kuwa mwamuzi wa mambo ya kifedha kwenye
kampuni yake.
Baadaye Rich aliingiwa na tamaa na kuanza kuwa na uhusiano na msichana mdogo aitwaye Iyake.
Ilikuja kugundulika kuwa mke wake anashindwa kupata
mimba kwasababu alikuwa akisimbuliwa na tatizo la Fibroid.
Rich anadaiwa kumshawishi mke wake akafanyiwe upasuaji wa
kuondoa tatizo naye akakubali.
Ripoti inasema mke wake alifariki muda mfupi baada ya
upasuaji huo kwa madai kuwa Rich alimtembelea hospitali na kumpa kidonge bila
ruhusa ya daktari kwa kudai kuwa kidonge hicho kingempunguzia maumivu bila
kujua kuwa ilikuwa sumu.
Baada ya daktari kubaini kuwa mikono yake ilikuwa salama
aliagiza kufanyike uchunguzi kwa mwili wa mwanamke huyo na ukabaini kuwa alipewa
sumu.
Sumu hiyo ilionesha kuwekwa katika muda ambao mume wake
alikuwa amekwenda kumsalimia kabla ya kufariki mke wake.
Muigizaji huyo alikuja kukiri kumuua mke wake baada ya
kupokea mateso makali kutoka kwa polisi.
No comments:
Post a Comment