Wamiliki wa simu fake nchini Kenya ambazo
kwa hapa bongo zimepewa jina la (simu za mchina), wana siku 10 tu za kuendelea
kufanya mawasiliano kwa kutumia simu hizo.
Tume ya Mawasiliano ya Kenya (CCK) imesisitiza
kuwa itazima mawasiliano ya simu zote zitakazobainika kuwa ni fake mwisho wa
mwezi huu wa September 2012.
Mkurugenzi Mkuu Francis Wangusi alisema
hakutakuwa na ongezeko la muda wa matumizi ya simu hizo.
"simu zote bandia zitakuwa switched
off September 30 2012, na baada ya hapo hatutaongeza tena muda wa simu hizo
kuendelea kutumika," alisema Wangusi.
Akihutubia mkutano wa waandishi wa habari
mjini Nairobi, alisema Wangusi njia zote zinazotakiwa zimefuatwa katika
kutekeleza agizo hilo.
Wangusi alisema lengo miongoni mwa masuala
mengine, ni kulinda nchi ya Kenya kutokana na tishio la uhalifu ugaidi, na
vurugu za kisiasa.
Aliongeza hoja pia kulinda walaji na
kulinda mafanikio yaliyopatikana hadi sasa katika sekta ya simu, mawasiliano ya
simu, hususani katika suala kwa simu mifumo ya malipo ya fedha.
Kwa mujibu wa CCK, karibu simu za mkononi million
3 zilizopo katika soko la Kenya ni bandia, ambayo ni sawa na asilimia 10% ya simu
zote zinazotumika nchini Kenya.
Haya ni baadhi ya maoni ya raia wa Kenya walivyolipokea swala hilo:
No comments:
Post a Comment