DMX |
Rapper mwenye sauti ya kipekee hasa kwenye
miondoko ya Hip Hop DMX, ameweka wazi kuwa ameshindwa kabisa kuendana na ukuaji
wa sayansi na teknolojia kwa sababu hawezi kabisa kutumia computer, iwe desktop
ama laptop.
DMX ambae ni member wa zamani wa kundi la
Ruff Ryder amesisitiza kuwa hana uwezo
kabisa wa kutumia laptop wala desktop computer, kitu ambacho kwa ulimwengu huu
sio cha kawaida hasa kwa mtu kama yeye mwenye jina kubwa na ambae habari
zake nyingi zinazomhusu zinatokea sana kwenye mitandao mbali mbali.
Sio kwamba hana uwezo wa kujifunza zaidi
kwa sababu elimu haina mwisho, lakini yeye hataki hata kujifunza kuhusu
matumizi ya computer, na kila anapoiangalia computer anaona kama ina vitu vya
kuogofya. Katika interview aliyofanya na Power 105.1 X alisema “angalia vitu vyote hivi, it’s scary, ina
mambo mengi mno, naapa kwa jina la bibi yangu kweli tena hadi nashindwa kuwa
mvumilivu kiasi hiki..Errr!ningeweza hata kuivunja” alisema DMX.
Hakuishia hapo akaongezea kuwa yeye kwake
Google hata haina maana kabisaaa, na haimuingii akilini ni kama kichekesho
flani, “it’s funny, it’s weird”.
Alipoulizwa yeye akitaka kuchek habari
zinazomhusu yeye mwenyewe inakuaje kama anaogopa computer na hajui kuitumia,
alisema yeye huwa anatumia simu yake na ndiyo anaielewa na sio laptop na
desktop computer, “I know how to do it on a phone”.
DMX anaweza kuwa sio rappa pekee ambae
ametamka hadharani kuwa hana ukaribu sana na hii teknolojia inayokuwa, wapo
wengi ambao hata mambo ya tweeter kwao wanaona hayana maana, kama utakumbuka
pia hasimu wa DMX kwa sasa na rapper wa Young Money Drake, aliwahi kukiri kuwa
hakuwa na urafiki na internet enzi hizo bado anatafuta jinsi ya kutoka akiwa
anafanya mixtape tu, hata nyimbo za 50 Cent na Kanye West alikuwa na CD zao na
sio soft copies, lakini yeye alikiri jinsi internet ilivyomsaidia sana, ambapo
nyimbo zilizokuwa kwenye Mixtape yake zilipoingia tu kwenye internet sauti yake
ikakita kwenye sikio la boss wake wa Young Money Lil Wayne na kwa jinsi alivyomteka
attention Lil Wayne akamsaka na kum-sign Young Money.
No comments:
Post a Comment