Kwa muda mrefu matajiri wengi walitamani kulinunua jumba la
kifahari la marehemu Michael Jackson ambalo pia linakumbukumbu kubwa kwa kuwa
ndipo alipofia mfalme huyo wa Pop, sasa jumba hilo limepata mnunuzi na
limeshalipiwa mkwanja wote unaostahili.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ jumba hilo limenunuliwa na
Steven Mayer ambae ni tajiri mkubwa na muwekezaji katika masuala ya bank.
Vyanzo mbalimbali vinaonesha kuwa jumba hilo limeuzwa kati ya
dola za kimarekani million 17 na dola million 20, na lilikuwa limepangwa kuuzwa
karibia dola za marekani million 24, ambazo zikibadilishwa kwa shilingi za
kitanzania yatakuwa mabilioni kibao.
Inaonesha kuwa mnunuzi huyo anahamu kubwa ya kuingia katika
jumba hilo kiasi kwamba amehamia wiki moja kabla ya umiliki wa mtu
aliyekabidhiwa kuiangalia haujafungwa rasmi.
Kinachofurahisha zaidi ni kwamba muuzaji nae amemruhusu Mayer
ahamie kwenye jumba hilo hata kabla hajasitishiwa rasmi umiliki ama uangalizi
wa jumba hilo la kifahari, japokuwa anasitasita kwa kuwa anaona ni risk kwake.
No comments:
Post a Comment