Wakati watu wamenogewa na show, Madonna
alistop kidogo na kuuliza, “nani ambae amejiandikisha kupiga kura?” Ikawa kama
amepata ngazi ya kuendelea, “sijali nani mtakaempigia kura as long as mtampigia
kura Obama.” Hapo baadhi ya mashabiki wakaanza kumzomea na wengine kuondoka na
kuisusia concert yake.
Madonna alionekana kutokujali akaendelea,
“seriously, sijali nani mtakaempigia kura…usiichukulie poa hii haki ya msingi.
Nenda kapige kura.”
Inaonekana kabisa Madonna yuko serious na
kumpigia kampeni Obama kila anapoona watu anaoamini ni wapiga kura kwa sababuu
hii haikuwa mara ya kwanza kuwahamasisha watu waliohudhuria tamasha lake, labda
nao wamechoshwa na maneno yake ya siasa.
Mwezi ulioopita alipokuwa Washington DC
alitumia muda wake kuwazungumzia viongozi wa zamani kama Abraham Lincoln na
Martin Luther King, Jr., akisema, “they killed him, as they do. … Ni ajabu
kufikiria kuwa tuna rais ambae ni African-American ndani ya White House. Hao
binadamu wema hawakufa for nothing.”
Ni kama muendelezo hivi kwa sababu majuzi
kati Watu wengi ‘walimkritisaizi’ Madonna kwa kumuita Obama Muislam mweusi
ndani ya White house alipokuwa katika tamasha lake kama kawaida. Lakini yeye mwenyewe
alivunja ukimya na kuelezea, “nilikuwa Ironic nilipokuwa jukwaani. Kweli najua
kabisa kuwa Obama sio muislam japo najua watu wengi hapa nchini wanaamini ni
muislam. Na vipi kama angekuwa muislam? Point yangu ni kwamba mtu mzuri ni
mzuri tu haijalishi anaabudu nini.
Sijali Obama ni dini gani- na wala mtu yeyote wa Marekani hatakiwi kujali
kuhusu hili.
No comments:
Post a Comment