Miezi kadhaa iliyopita Timbulo aliandamwa na maswali mengi yaliyoambatana na maneno ya kumshutumu kuwa ali copy na kupaste nyimbo zake mbili zilizopita "Domo Langu" na "Waleo Wakesho" kutoka katika nyimbo za kundi hilo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Timbulo alidai kuwa haku copy bila idhini ya wenye nyimbo kama inavyodhaniwa na wengi, bali alipewa ruhusa na X-Maleya wenyewe na vithibitisho vyote anavyo.
Timbulo ameendelea kusema kutokana na kwamba anawa feel sana X-maleya na wao wanam feel, sasa ameamua kuwashirikisha kabisa katika wimbo wake mpya aliouita "Lastic ya Upendo" inayotegemewa kutoka hivi karibuni na tayari wameshamtumia demo yenye sauti zao na ya Timbulo na kinachosubiriwa sasa ni mixing imalizike.
Kupitia ukurasa wake wa facebook Timbulo leo ameandika: " Habar njema ni kwamba wimbo mpya tayar upo mkonon, waitwa Lastic ya upendo nimefanya na x-maleya, a group music from cameroun, ambao nimewah kutajwa kuiba nyimbo kutoka kwao,,,!".
Leotainment ilimuuliza Timbulo juu ya mpango wa video ya wimbo huu aliyowashirikisha wasanii kutoka nje ya Tanzania, na hiki ndicho alichojibu:
" Wao X-maleya walitupa option tatu za kufanya video, option ya kwanza ni wao watutumie clips za parts zao walizoimba katika wimbo huu watakazo shot huko kwao. Option ya pili ni sisi tusafiri kwenda Cameroon kushot huko, na option ya tatu ni wao waje Tanzania tushot hapa. Sasa mpango mzima utafahamika mara baada ya audio ya wimbo huu kuwa released wiki ijayo kama mixing na mastering itakuwa imekamilika, lakini uamuzi wa kufanya video utatoka katika hizo option tatu".
Kazi hii ya "Lastic ya upendo" imetengenezwa katika studio ya Combination Sound chini ya producer Man water, lakini mixing inafanyika hapa Tanzania na Cameroon kisha watachagua ile itakayokuwa nzuri zaidi kwa ajili ya official release.
No comments:
Post a Comment